Mwongozo huu unatoa maelekezo ya hatua kwa hatua kuhusu jinsi ya kutekeleza miamala ya multisig [multisig transactions] kwa kutumia Zkool. Unajumuisha kuunda akaunti, kutuma au kupokea fedha, na kusanidi utengenezaji wa funguo uliosambazwa (DKG) kwa multisig. Picha za skrini zimejumuishwa kwa kila hatua kuu.
Mafunzo
1. Kuunda Akaunti
Fungua programu ya Zkool na uende kwenye Akaunti Mpya.
Weka Jina la Akaunti (kwa mfano Anabelle).
Kwa hiari, washa au zima Tumia Mabadiliko ya Ndani au Rejesha Akaunti ikihitajika.
Baada ya kuundwa, akaunti itaonekana katika Orodha yako ya Akaunti.
2. Kupokea Fedha
Kila akaunti hutengeneza aina nyingi za anwani:
Anwani Iliyounganishwa
Anwani ya Orchard pekee
Anwani ya Sapling
Anwani ya uwazi [Transparent Address]
Chagua aina unayotaka kutumia na uishiriki ili kupokea fedha.
3. Kutuma Fedha
Nenda kwenye sehemu ya Mpokeaji.
Weka anwani ya mpokeaji.
Bainisha kiasi na ujumbe [memo] wa hiari.
Kagua maelezo ya muamala [transaction] na thibitisha.
Baada ya kukamilika, salio husasishwa katika orodha yako ya akaunti.
4. Kutekeleza Miamala ya Multisig: Kusanidi Utengenezaji wa Funguo Uliosambazwa (Multisig)
Multisig katika Zkool hutumia Utengenezaji wa Funguo Uliosambazwa (DKG) ili kuhakikisha washiriki wengi wanadhibiti akaunti ya pamoja.
Hatua ya 1: Anzisha DKG
Chagua Jina la pochi ya pamoja [shared wallet] (kwa mfano Anabelle).
Weka Idadi ya Washiriki.
Chagua Kitambulisho chako cha Mshiriki.
Bainisha Idadi ya Watia Saini Inayohitajika (Kizingiti).
Chagua Akaunti ya Ufadhili.
Hatua ya 2: Ongeza Anwani za Washiriki
Weka Anwani Iliyounganishwa ya kila mshiriki (inapendekezwa).
Dokezo [Note]: Ukitumia anwani ya Orchard pekee au Sapling pekee, multisig itakuwa na ukomo kwa bwawa hilo pekee [pool] (Orchard au Sapling).
Hii inamaanisha pochi ya pamoja haiwezi kupokea fedha kutoka mabwawa mengine.
Kwa uoanifu na unyumbufu wa juu zaidi, tumia daima Anwani Zilizounganishwa.
Hatua ya 3: Endesha Raundi za DKG
Subiri washiriki wote wabadilishane vifurushi vya raundi ya 1 na raundi ya 2.
Hatua ya 4: Kamilisha Anwani ya Pamoja
Baada ya kukamilika, anwani ya pamoja hutengenezwa.
Hitimisho
Kwa kutumia Zkool, unaweza: kuunda akaunti, kutuma na kupokea fedha, na kusanidi pochi ya multisig kwa kutumia Utengenezaji wa Funguo Uliosambazwa. Hii huhakikisha usalama ulioimarishwa na usimamizi shirikishi na wa faragha wa fedha.