Brave Wallet ni pochi ya kripto [wallet] salama, asilia iliyojengwa moja kwa moja kwenye kivinjari cha Brave - hakuna viendelezi vinavyohitajika.
Zcash ni mojawapo ya sarafu za kripto chache zinazotoa faragha [privacy] kwa chaguo-msingi kupitia miamala ya faragha [transactions].
Brave Wallet sasa inasaidia Orchard za faragha za ZEC, ikiwezesha miamala ya kibinafsi bila programu ya wahusika wengine.
Watumiaji sasa wanaweza kutuma/kupokea ZEC bila kufichua salio au metadata - yote ndani ya kivinjari cha Brave.
Hatua zinazojumuishwa:
Fungua Kivinjari cha Brave (kwa kompyuta ya mezani pekee kwa sasa)
Bofya aikoni ya Pochi au nenda kwenye brave://wallet
Sanidi pochi yako (unda au ingiza)
Fikia dashibodi ya kripto

Hatua zinazojumuishwa:
Kwenye dashibodi ya Pochi, bofya “Dhibiti Rasilimali”
Tafuta ZEC na uiwashe
ZEC sasa inaonekana kwenye pochi yako

Hatua zinazojumuishwa:
Bofya ZEC katika rasilimali zako
Chagua “Pokea”
Brave hutengeneza Anwani Jumuishi (UA) - anwani [address] moja inayosaidia miamala ya faragha na miamala ya uwazi [transparent]
Nakili au changanua msimbo wa QR
Shiriki UA yako na mtumaji

Hatua zinazojumuishwa:
Chagua ZEC -> Tuma
Bandika Anwani Jumuishi ya mpokeaji au anwani ya faragha
Weka kiasi
Thibitisha maelezo ya muamala
Bofya Tuma - fedha sasa zinahamishwa kwa faragha, kwa kutumia bwawa la Orchard

Hapa kuna maelezo kwa kila aina ya anwani ya Zcash:
t-addr (t1...) - Anwani za uwazi hufanya kazi kama anwani za Bitcoin, kumaanisha miamala ni ya umma kwenye blockchain. Ni rahisi zaidi kutumia na pochi zisizo za Zcash lakini hazitoi faragha.
z-addr (zs...) - Anwani za faragha hutumia teknolojia ya faragha ya Zcash (Sprout/Sapling) kuficha mtumaji, mpokeaji na kiasi. Ni funguo za kutazama [viewing keys] au mmiliki pekee wanaoweza kufichua maelezo.
UA (u... or QR) - Anwani Jumuishi huunganisha aina nyingi za anwani (za uwazi, za faragha, Orchard) kuwa moja. Hii huruhusu uoanifu wa juu zaidi huku ikipendelea faragha inapowezekana.
Kwa kutumia Brave Wallet na ZEC za faragha, faragha sasa inapatikana kwa kila mtu - hakuna programu maalumu au maarifa ya juu yanayohitajika.
Inafaa kwa waandishi wa habari, wanaharakati, au watu wanaojali faragha.
Jaribu muamala wako wa kwanza wa faragha leo ndani ya Brave!
Dumisha faragha. Dumisha uhuru. Tuma ZEC kwa faragha ukitumia Brave Wallet.