
Free2Z: Usanidi wa akaunti + Mafunzo ya utiririshaji mubashara
Utangulizi
Free2Z ni jukwaa linalowaunganisha watayarishi na waungaji mkono ili kuwasiliana na kutimiza malengo yao. Free2Z hutoa vifaa [tools] kwa watayarishi kuonyesha vipaji vyao na kukusanya fedha kwa ajili ya miradi yao bila kuathiri faragha [privacy]. Waungaji mkono wanaweza kupata na kuunga mkono malengo wanayoyaamini.
Unda akaunti yako
Kwa sasa, kuna njia mbili za kuunda akaunti yako kwenye Free2Z:
- Chagua jina la mtumiaji na nenosiri.
- Unganisha akaunti yako ya Twitter.
Ili kuunda akaunti au kuingia, tembelea https://free2z.cash/ na ubofye kitufe cha “UNDA”.

Fomu ya kuingia/kujisajili itaonekana kwenye kivinjari chako. Chagua jina lako la mtumiaji na nenosiri imara - haya yatakuwa maelezo yako ya kuingia. Tatua captcha na ubofye kitufe cha “Ingiza” ili kuunda akaunti yako.

Vinginevyo, unaweza kuunda akaunti ya Free2Z kwa kuunganisha akaunti yako ya Twitter. Ili kufanya hivyo, bofya nembo ya Twitter iliyo karibu na “Ingia Kwa Kutumia”, na utaombwa kuunganisha akaunti yako ya Twitter.

Bofya Idhinisha programu ili kuunganisha akaunti yako ya Twitter na Free2Z.
Binafsisha wasifu wako
Baada ya akaunti yako kuundwa, utaelekezwa kwenye ukurasa wako wa wasifu wa Free2Z. Ikiwa uliunda akaunti yako kwa kuunganisha Twitter yako, sehemu nyingi zitajazwa kiotomatiki. Ikiwa uliunda akaunti kwa kuingiza jina la mtumiaji na nenosiri, unapaswa kuingiza maelezo yako hapa. Unaweza kutumia jina bandia badala ya jina lako halisi.

Kwa sasa inaonekana ya kuchosha, kwa hiyo tuifanye ivutie zaidi kwa kuweka picha ya utambulisho na bango. Kiolesura cha Free2Z hurahisisha sana hatua hii kwa kutumia kitufe cha kupakia (mshale wa juu upande wa kulia).

Unaweza kuona matokeo juu ya ukurasa.

Ah, bora zaidi! Ikiwa una ujuzi wa kisanii, unaweza kuufanya ukurasa wako wa wasifu wa Free2Z uonekane wa kuvutia sana! Andika maelezo mazuri kwa ajili ya ukurasa wako. Unaweza kuzungumzia kuhusu wewe mwenyewe au kueleza aina ya maudhui ambayo wengine wanaweza kutarajia kutoka kwako. (Dokezo: Tumia sintaksia ya markdown kubinafsisha maelezo yako!)

Usisahau kutoa anwani yako ya faragha [shielded address] ya Zcash, ili waungaji mkono waweze kukutolea michango moja kwa moja!

Hatua ya mwisho ya kukamilisha usanidi wa ukurasa wako ni kuweka “Bei ya Mwanachama”. Hii ni bei katika 2Zs (Tuzies) ambayo watumiaji wengine watalipa ili kujiandikisha kwenye ukurasa wako! (Zaidi kuhusu 2Zs baadaye).

Hatimaye, bofya kitufe cha “Sasisha Wasifu” ili kukamilisha usanidi wa wasifu wako!
Usajili na 2Zs
Free2Z huwaruhusu watumiaji kujiandikisha kwa watayarishi wanaowapenda na kupata vipengele vya kipekee na maudhui ya wanachama pekee. Mtayarishi anapaswa kusanidi kiwango cha chini cha 2Zs kwa ajili ya usajili.
2Zs au Tuzies ni mikopo ya kidijitali ya ndani ya programu inayotumika katika Free2Z kwa madhumuni mengi, yakiwemo:
- Kujiandikisha kwa watayarishi
- Kuongeza mwonekano wa ukurasa wa Free2Z
- Kutoa michango kwa watayarishi
Unaweza kuona mikopo yako ya 2Zs kwenye kichwa cha ukurasa wako wa wasifu.

Unaweza kununua 2Zs zaidi kwa kutumia Zcash kwa kubofya salio lako la 2Zs. Kiwango cha chini cha ununuzi ni 0.05 ZEC, na kiwango cha sasa cha ubadilishaji ni 0.05 ZEC = 10 2Zs.

Kutoa michango na kujiandikisha
Mara tu unapompata mtayarishi unayempenda, unaweza kuonyesha shukrani yako kwa kumtolea mchango na kujiandikisha kwake. Michango yote huenda moja kwa moja kwenye pochi [wallet] ya mtayarishi. Kwa mfano, tujiandikishe kwenye ukurasa wa Free2Z mwenyewe.

Ili kujiandikisha kwenye ukurasa, unachohitaji kufanya ni kubofya ikoni ya kujiandikisha kwenye kichwa cha ukurasa.

Utaona kiwango cha chini cha kujiandikisha. Thibitisha kama una tuzis za kutosha na ubofye jiandikishe.

Toa mchango kwa kutumia 2Zs au Zcash
Unaweza kutoa mchango moja kwa moja kwenye ukurasa wao, kwa kubofya ikoni ya Kufadhili mtayarishi.

Au, kutoka ndani ya chapisho, tafuta kitufe cha kuelea chenye alama ya kuongeza. Kutoka hapa, unaweza kutoa mchango kwa mtayarishi au kukuza chapisho kwenye Free2Z.

Utiririshaji Mubashara
Jukwaa la Free2Z hutoa kipengele bora kinachoitwa Free2Z Live. Kwa kifaa hiki, watayarishi wanaweza kuanzisha mitiririko mubashara kwa wanachama waliojiandikisha. Baadhi ya vipengele muhimu vya Free2Z Live ni:
- Sauti na video
- Kushiriki skrini
- Kuhariri msimbo kwa ushirikiano
- Gumzo
- Ubao mweupe
- Na mengi zaidi!
Unaweza kufanya nini kwa kutumia Free2Z Live
Free2Z Live ni kifaa chenye uwezo mkubwa, kinachowaruhusu watayarishi kutiririsha aina yoyote ya maudhui. Hii hapa ni mifano michache ya aina za maudhui unazoweza kutiririsha kwa kutumia Free2Z Live:
- Mafunzo na maonyesho
- Maonyesho ya kisanii na matukio
- Miradi ya ushirikiano
- Utoaji wa taarifa mubashara na uandishi wa habari
- Ubunifu wako ndio kikomo!
Jinsi ya kuanza moja kwa moja
Ni rahisi sana kuanzisha utiririshaji mubashara kwa kutumia Free2Z Live. Lakini kuna mahitaji machache kabla ya kuanza utiririshaji wako.
- Mtayarishi lazima awe na bei ya mwanachama ya chini ya 10 2Zs.
- Mtayarishi lazima awe na salio la angalau 150 2Zs kwenye akaunti yake.
Ikiwa mtayarishi anatimizia masharti yote mawili yaliyo hapo juu, ikoni inayoitwa Anza Mubashara itapatikana kwake kwenye ukurasa wake wa wasifu.

Ili kuanzisha utiririshaji mubashara, bofya tu kitufe cha Anza Mubashara, na programu ya Free2Z itaomba ruhusa ya kutumia maikrofoni yako na kamera yako ya wavuti (ikiwa unayo). Baada ya kutoa ruhusa zinazohitajika, Free2Z itakuomba uingize jina la utani unalotaka kutumia wakati wa utiririshaji mubashara. Baada ya kuchagua jina la utani, bofya Jiunge ili kuanzisha utiririshaji wako mubashara.

Na imekamilika! Unapoanzisha utiririshaji mubashara, wasifu wako utaonyesha ikoni inayoashiria kwamba uko mubashara, ili waliojiandikisha kwako waweze kujiunga na utiririshaji mubashara.

Watu wanapojiunga na utiririshaji mubashara, wanaweza kupiga gumzo, kuomba kujiunga na jukwaa, kuingiliana kwa kupiga kura katika kura za maoni, na mengine mengi.

(Mfano wa kipindi cha Free2Z Live)
Free2Z Live ina matumizi mengi na uwezo mkubwa. Katika sehemu inayofuata, nitatoa muhtasari wa utendaji na vifaa vyake.
Kuchunguza Free2Z Live
Hati hii ya wiki haikusudiwi kuwa mwongozo wa kina wa Free2Z au Free2Z Live. Lakini huu hapa ni muhtasari wa jumla wa vifaa vyake.
Katika sehemu ya chini kushoto ya skrini, tunaona vitufe vichache.

Kazi nzuri hapa ni uwezo wa kushiriki skrini yako ili watumiaji wengine waweze kuona unachofanya.
Chini tunaweza kupata chaguo za utiririshaji mubashara.

Baadhi ya chaguo muhimu hapa ni:
- Kunyamazisha / kuwasha maikrofoni
- Kuwasha / kuzima kamera ya wavuti
- Kuondoka kwenye jukwaa
- Kunyamazisha wazungumzaji wote
- Kuondoka
Ili kumaliza utiririshaji mubashara, unapaswa kubofya kitufe cha “Ondoka”, kisha ubofye “Maliza mkutano kwa wote” ili kusimamisha mkutano kwa washiriki wote.

Vitufe vya chini kulia vina kazi zinazohusiana na mwingiliano wa utiririshaji mubashara, kama vile:
- Gumzo: Hii huwaruhusu washiriki kupiga gumzo wao kwa wao na mwenyeji wakati wa utiririshaji mubashara.
- Kura za maoni: Hii humruhusu mwenyeji kuunda kura za maoni na kukusanya maoni kutoka kwa washiriki.
- Orodha ya washiriki: Hii huonyesha orodha ya washiriki katika utiririshaji mubashara.
- Programu-jalizi: Hii humruhusu mwenyeji kuongeza programu-jalizi na viendelezi ili kuboresha uzoefu wa utiririshaji mubashara.

Si kusudi la hati hii ya wiki kueleza programu-jalizi zote, lakini ninakuhimiza sana ujaribu kila moja, kwa kuwa zote hutoa thamani kubwa ya mwingiliano kati ya watayarishi na watazamaji. Ili kuzindua programu-jalizi, bofya tu kitufe cha “roketi” kilicho upande wa kulia.
Hitimisho
Kwa hitimisho, Free2Z ni jukwaa lenye matumizi mengi kwa watayarishi kuonyesha uwezo wao, kushiriki maarifa na kukusanya fedha kwa ajili ya miradi yao, na kushirikiana na waungaji mkono wao kupitia kifaa chenye uwezo mkubwa cha Free2Z Live.
Rasilimali
Free2Z
Nyaraka za Free2Z
Muhtasari wa 2Z
Kuunda wasifu
Free2Z Live ni nini?
Free2Z kwa Waungaji Mkono
Imeandikwa na James Katz kwa ajili ya ZecHub.