Kuona Anwani za Zcash
Ikiwa unajifunza kuhusu Zcash kwa mara ya kwanza, utagundua mara moja kwamba kuna aina mbili za miamala [transactions] inayoweza kutokea: ya uwazi [transparent] na ya faragha [shielded].
Zaidi ya hayo, ikiwa umekuwa ukifuatilia maendeleo ya hivi karibuni katika mfumo ikolojia wa Zcash, huenda umejifunza kuhusu Anwani Zilizounganishwa, au UA.
Watu katika tasnia ya Zcash wanapozungumzia miamala ya faragha, wanamaanisha miamala inayohusisha anwani ambazo zimesimbwa kwa itifaki za Sapling au Orchard.
UA zimeundwa kuunganisha muamala wa aina yoyote wa faragha au wa uwazi katika anwani moja. Ujumlishaji huu ni ufunguo wa kurahisisha UX katika siku zijazo. Madhumuni ya mwongozo huu ni kuongeza uelewa wa UA kwa mifano thabiti ya kuona.
Aina za anwani za Zcash
Kwa sasa kuna aina tatu kuu za anwani zinazotumika hadi leo. Hizi ni pamoja na


- Anwani Iliyounganishwa (Kamili)

Jambo la kwanza la kutambua ni kwamba urefu wa kila aina ya anwani ni tofauti. Unaweza kuona hili kwa idadi ya herufi katika mfuatano wa anwani au kwa kuangalia misimbo ya QR inayohusishwa. Urefu wa anwani unapoongezeka, msimbo wa QR huwa unapungua kwa taswira na kutoshea data zaidi katika mraba.
t1goiSyw2JinFCmUnfiwwp72LEZzD42TyYu ina herufi 35
zs1cpf4prtmnqpg6x2ngcrwelu9a39z9l9lqukq9fwagnaqrknk34a7n3szwxpjuxfjdxkuzykel53 ina herufi 78
u1ckeydud0996ftppqrnpdsqyeq4e57qcyjr4raht4dc8j3njuyj3gmm9yk7hq9k88cdkqfuqusgpcpjfhwu3plm2vrd32g8du78kzkm5un357r4vkhz4vhxd4yfl8zvszk99cmsc89qv4trd7jzkcs8h6lukzgy25j8cv76p0g603nrrg6yt6cxsh2v8rmkasskd69ylfyphhjyv0cxs ina herufi 213
Jambo la pili la kutambua ni kiambishi awali cha kila mfuatano wa anwani -- anwani za uwazi huanza kwa t, Sapling kwa zs, na hatimaye UA kwa u1.
Ni muhimu kutambua:
"Anwani za malipo [payment] za Orchard hazina usimbaji wa mfuatano unaojitegemea. Badala yake, tunafafanua "anwani zilizounganishwa" ambazo zinaweza kujumuisha pamoja anwani za aina tofauti, zikiwemo Orchard. Anwani zilizounganishwa zina Sehemu Inayosomeka kwa Binadamu ya "u" kwenye Mainnet, yaani zitakuwa na kiambishi awali "u1". "
Vipokezi vya Anwani Iliyounganishwa
Kama ilivyojadiliwa hapa, mtu anaweza kujenga UA zenye vipokezi tofauti -- mchanganyiko fulani wa aina za anwani za uwazi, Sapling, na Orchard.
Kando na UA kamili, hizi ndizo zinazopatikana kwa kawaida zaidi:




Jambo la kwanza la kutambua ni kwamba UA hizi zote zinatokana na ufunguo sawa wa faragha! Jambo la pili la kutambua ni urefu wa kila aina ya UA:
- t+s
u13qutpuktq026dwczvxmnh8mxdacsjx3kg2rrhzgns8zsty53t9y0hqp5d440zc9w7z7zkkjqw8dq0uuc0mkt883464mq8mkys7l4xjnhylh7u3u02ukknurm5yxerqlf500y2atq28e herufi 141
- t+o
u1yvwppp7ann6n3pgkysdu0spvr50w4jf4jwgme3c8x8fp4av59rupgvdd3fddc3f2cwrk3ghs5lxt87ggj8cvjuzcrf4jkejwlu9pc83gk2vtx03ucqcc3ed0furcuypqs6d6swu3nws herufi 141
- s+o
u1dq8kg78fgpjsc7dn2ynpdzc8xu99wra0jec4jy30rjqk5frsj62qtgqcu9nn0j8g352phlwprshancgxcuhdcclx0wxtvqylhmuegas7ul8hwnwggy727l05pyujuywtnn4nkfznctaelpkcrqcm9cxhkgv3t9jtrvgym7la5varrmzc herufi 178
- o
u1cysntkxwt0h4sahp7rhj7u27pgc2ga7685ekf65g0d5ht5glkfm4zkumhvkd2zg2pdrgv3mrwq2x3vw2yl5u7zef3cr2nqwrzu7v2dsa herufi 106
Jambo la tatu la kutambua ni kwamba, kwa taswira, kila UA ni tofauti kidogo! Nguvu ya UA ni uchaguzi unaoruhusu watumiaji wa mwisho. Ikiwa itifaki mpya itahitajika katika siku zijazo, UA zitakuwa tayari kutumika.
Vyanzo
https://zcash.github.io/orchard/design/keys.html
https://medium.com/@hanh425/transaction-privacy-78f80f9f175e