Ya faragha [Shielded] dhidi ya Uwazi [Transparent]
Kwa hali ilivyo sasa, kuna aina mbili za anwani [addresses] na miamala [transactions] katika Zcash, za faragha [shielded] na za uwazi [transparent]. Tofauti kati ya ZEC ya faragha na ya uwazi ni rahisi sana. ZEC ya faragha huweka pesa zako na miamala yako kuwa ya faragha, ilhali ZEC ya uwazi hufanya kazi kama Bitcoin, kwa uwazi kamili. Hii inamaanisha kwamba mtu anaweza kuona salio lako na miamala yako yote ikiwa anajua anwani yako.
Watu wanapoanza kutumia ZEC kwa mara ya kwanza, huenda wasitambue ni aina gani ya anwani wanayotumia. Hii ni kwa sababu si masoko yote ya kubadilishana sarafu [exchanges] yanaunga mkono ZEC za faragha na/au utoaji wa ZEC za faragha.
Kwa hiyo, kwa mfano, ikiwa mtu anatumia Coinbase na kununua ZEC, angenunua ZEC ya uwazi na angeweza tu kutoa ZEC hiyo kwenye anwani ya uwazi katika pochi [wallet]. Pochi kama Zodl zinaweza kufanya fedha zilizotumwa kwenye anwani ya uwazi kuwa za faragha ili kutatua hili, lakini si kila mtu anayefahamu hilo. Kwa ufupi, watu wengi hutumia ZEC kwa namna ambayo soko lao la kubadilishana sarafu au pochi yao kuu inawaruhusu kutumia.
Kuhakikisha kwamba ZEC yako ni ya faragha
Tunapendekeza kila mtu ajihifadhie ZEC yake mwenyewe. Hii inamaanisha kuhamisha ZEC yako kutoka kwenye soko la kubadilishana sarafu hadi kwenye pochi. Njia bora ya kujua ikiwa unatumia ZEC ya faragha, yaani ya binafsi, ni kuangalia anwani ambamo salio lako lipo. Ikiwa anwani inaanza kwa “z” au “u1”, basi salio lako ni la faragha. Ikiwa anwani inaanza kwa “t”, basi salio ni la uwazi.
Kwa ujumla kuna njia mbili za kupata ZEC ya faragha.
Kutoka kwenye soko la kubadilishana sarafu linalounga mkono utoaji wa faragha:
Nunua ZEC kwenye soko la kubadilishana sarafu
Anzisha mchakato wa utoaji kwenye soko la kubadilishana sarafu
Fungua pochi yako ya ZEC ya faragha na uhakikishe kuwa anwani ya kupokea inaanza kwa “u1” au “z”
Tekeleza utoaji kutoka kwenye soko lako la kubadilishana sarafu
Kutoka kwenye soko la kubadilishana sarafu linalounga mkono utoaji wa uwazi:
Nunua ZEC kwenye soko la kubadilishana sarafu
Anzisha mchakato wa utoaji kwenye soko la kubadilishana sarafu
Fungua pochi yako ya ZEC inayoweka fedha kiotomatiki kuwa za faragha [autoshielding] na utumie anwani ya uwazi ya kupokea
Tekeleza utoaji kutoka kwenye soko lako la kubadilishana sarafu
Subiri uthibitisho 10, kisha fanya ZEC kutoka anwani yako ya uwazi kuwa ya faragha katika anwani ya faragha
Hapa kuna mafunzo ya jinsi ya kutoa ZEC kutoka kwenye soko la kubadilishana sarafu. Kumbuka kwamba huu ni utoaji wa faragha.
Hapa kuna mafunzo ya jinsi ya kufanya ZEC yako kutoka anwani ya uwazi kuwa ya faragha katika anwani ya faragha.
Hapa kuna mafunzo ya jinsi ya kununua ZEC kwenye Coinbase na kuituma kwa Zodl.
Miamala
Baada ya kuhakikisha kwamba ZEC yako iko katika pochi ya faragha inayounga mkono anwani za faragha, sasa unaweza kuamua ikiwa ungependa kufanya miamala kwa kutumia ZEC hiyo. Kufanya miamala kwa kutumia ZEC ni rahisi sana. Unaweza kutuma ZEC kwenye anwani za faragha au za uwazi kulingana na upendeleo wa mtu anayepokea. Kama ilivyo kwa muamala wowote wa kifedha, kuna uwezekano mdogo wa watu kuvuja data. ZEC ni bora zaidi katika kupambana na uvujaji wa data, lakini hiyo haimaanishi kwamba unapaswa kuitumia bila uangalifu. Haya ni baadhi ya mambo unayopaswa kuepuka unapofanya miamala kwa kutumia ZEC.
Kufichua anwani yako ya faragha
Kutumia anwani ya faragha kama njia ya kupitisha kwa anwani za uwazi (yaani “uchanganyaji” [mixing])
Kuendesha, na kufichua kuwa unaendesha, idadi kubwa ya miamala ya kutoka faragha kwenda uwazi
Kuwajulisha watu mara kwa mara mahali unapotumia ZEC ya faragha
Kimsingi, jambo bora la kufanya kwa ZEC yako ni kuihifadhi katika pochi ya faragha, kufanya miamala kati ya anwani za faragha, na kuwa makini kuhusu jinsi unavyotumia ZEC hadharani (yaani, kwenye duka la kahawa). Kuhakikisha faragha kunakuja na kiwango fulani cha wajibu.