ZecHub
Anza Hapa
Anza safari yako ya kujifunza Zcash
ZecHub
Anza Hapa
Anza safari yako ya kujifunza Zcash
Watu hutumia ZEC kufanya miamala [transactions] kwa ufanisi na usalama kwa ada [fees] ndogo. Mfumo wa faragha [Shielded] wa Zcash huhakikisha miamala inabaki kuwa ya siri, huku ukiwapa pia chaguo la kushiriki maelezo ya anwani [address] na muamala iwapo watachagua kufanya hivyo. Miamala ya faragha, ya “Z-Z”, huonekana kwenye blockchain ya umma ili ijulikane kwamba ilifanyika na kwamba ada zililipwa. Hata hivyo, anwani, kiasi cha muamala na sehemu ya ujumbe [memo] yote yamesimbwa fiche [encrypted] na hayaonekani hadharani.
Watu wanaweza pia kutumia ZEC kuhifadhi utajiri katika mali imara inayolinda faragha [privacy]. Kutakuwa na vitengo milioni 21 vya ZEC pekee, ikimaanisha kwamba mali hii ina ugavi usiobadilika. Baada ya kitengo cha 21 milioni cha ZEC kuingia kwenye mzunguko kupitia uchimbaji [mining] mined into circulation, mali hiyo itakuwa kinga dhidi ya mfumuko wa bei. Mali zinazokinga dhidi ya mfumuko wa bei ni kinga nzuri dhidi ya mfumuko wa bei iwapo walinda milango wa kati wataongeza ugavi wa fedha za kitaifa.
Watu wanaweza kutumia sehemu ya ujumbe katika muamala wa faragha wa Z-Z kutuma jumbe zilizosimbwa fiche kikamilifu. Ili kutuma ujumbe, watumiaji lazima wafanye muamala na walipe ada ya muamala, ambayo ni chini ya $0.01.