ZecHub
Anza Hapa
Anza safari yako ya kujifunza Zcash
ZecHub
Anza Hapa
Anza safari yako ya kujifunza Zcash
Msingi wa fedha wa Zcash ni sawa na ugavi usiobadilika wa Bitcoin wa vitengo vya sarafu (currency units) vya ZEC milioni 21. Kila sekunde 75, block mpya huchimbwa kwenye blockchain ya Zcash na zawadi ya block (block reward) ya ZEC 1.5625 huingizwa katika mzunguko. Zawadi hii ya block hugawanywa kwa wachimbaji (miners) na mfuko wa maendeleo (development fund) wa Zcash.
Kiasi cha zawadi ya block hupunguzwa kwa nusu takribani kila baada ya miaka minne hadi ZEC zote milioni 21 ziwe katika mzunguko. Mfumuko wa sarafu (inflation) wa Zcash karibu unaiga kwa usahihi ule wa Bitcoin. Ni muhimu kutambua kwamba kadiri sarafu mpya zinavyoundwa, mfumuko wa sarafu hupungua, na katika kila upunguzaji nusu (halvening) kiwango hupungua kwa kiasi kikubwa.