


Jopo la Ushauri la Jumuiya la Zcash, au ZCAP, ni jopo linaloundwa na wanachama wa Jumuiya ya Zcash, lililoanzishwa kama njia ya kuhusisha jumuiya na kuomba maoni yao ya ushauri kila wakati Zcash Foundation inapohitaji kufanya uamuzi unaohusu au unaoathiri jumuiya hiyo. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018, jopo hili limesaidia kubainisha mwelekeo wa Zcash Foundation katika maamuzi mengi muhimu, baadhi yake yakiwa:
Alama ya Biashara ya Zcash: Kura hii ilihusu kama Zcash Foundation inapaswa kutafuta makubaliano ya kisheria na Electric Coin Company (ECC) ya kugawana umiliki na udhibiti wa alama ya biashara ya Zcash
Sera ya Kifedha: Kura hii ilihusu kama Zcash Foundation inapaswa kutetea mabadiliko yoyote katika sera ya kifedha ya Zcash, kama vile kiwango cha utoaji, ratiba ya kupunguzwa kwa nusu [halving], au kiwango cha mfumuko wa bei
Upinzani dhidi ya ASIC: Kura hii ilihusu kama Zcash Foundation inapaswa kutanguliza upinzani dhidi ya ASIC kama thamani na lengo la mtandao wa Zcash
Uchaguzi wa Kamati ya Zcash Community Grants: Kura hii ilihusu kuchagua wanachama wawili wa kamati ya Zcash Community Grants (ZCG), ambayo ina jukumu la kupitia na kufadhili mapendekezo ya ruzuku [grant] kwa miradi inayohusiana na Zcash
Mpango wa Ruzuku Ndogo wa Zcash: Kura hii ilihusu kuidhinisha au kukataa maombi ya ruzuku kwa miradi midogo ya Zcash iliyotuma maombi ya ufadhili kutoka Zcash Foundation
Uenezaji na maendeleo ya Mali za Faragha za Zcash, ambayo huwezesha matumizi ya mali za jumla za DeFi ndani ya mfumo ikolojia wa Zcash ambao ni wa faragha kwa chaguo-msingi.
Uchaguzi wa wanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya Zcash Foundation
Wazo nyuma ya ZCAP ni kwamba inaundwa na kundi tofauti la wanajamii wenye mataifa, majukumu na maoni mbalimbali, ili kuhakikisha inasalia imejitolea kwa lengo lake la kuwakilisha sauti na maslahi ya watumiaji na washikadau wa Zcash, huku ikidumisha mtandao ulio wazi na tofauti.
Kufikia Oktoba 2023, ZCAP iliundwa na wanachama 188, na hupanuliwa mara kwa mara. Pia, Zcash Foundation ime“panua vigezo vya ustahiki wa uanachama wa ZCAP, ikijumuisha vigezo vilivyopendekezwa na wanachama wa jumuiya ya Zcash”.