



Cypherpunk Zero ni mfululizo wa simulizi unaomlenga Zero, mdukuzi mchanga wa cypherpunk na mpigania uhuru. Kwa sasa Zero anaishi katika jinamizi la jamii ya kidistopia, na anatumia msimbo kupambana na walinda-lango waliowekwa katikati wanaoifunga jamii pingu. Simulizi hili lilihamasishwa na kriptografia ya Zcash na Halo. Kazi hii ya ubunifu ni juhudi za ushirikiano kati ya ECC, Stranger World, Might Jaxx, na washirika teule wa mfumo ikolojia. Kazi hii ya ubunifu imelenga hasa mfululizo wa NFT wa , na toy ya kukusanywa ya pia imetolewa. Jumuiya ya NFT, ambayo ina shughuli nyingi zaidi kwenye Twitter, hata imeanzisha shirika lililogatuliwa [decentralized organization] (DAO) la ili kupanga na kukamilisha miradi inayounga mkono kampeni hii, pamoja na jumuiya pana ya Zcash.
Tumeona miradi mingi sana ikiahidi kupita kiasi na kutotekeleza ipasavyo ramani zake za njia za NFT. Kwa hiyo, hakuna ramani rasmi ya njia. Amini kwamba tuna manufaa ya ajabu na ya kipekee yanayoandaliwa kwa wamiliki wa NFT, baadhi yakitarajiwa na mengine yasiyotarajiwa. Jifungeni mikanda na muungane nasi katika safari hii.
Snapshot — tovuti maalumu ya DAO katika vote.cypherpunkzero.com ilisitishwa, na kikoa chake hakitatui tena; hii ndiyo nafasi ya Snapshot iliyosalia.
Jumla ya ugavi: NFT 10,000 za kipekee zinazozalishwa kwenye Ethereum Mainnet
4% ya ugavi (NFT 400 za kwanza) zilitolewa kwa njia ya airdrop kwa wafuasi wa awali wa miradi hiyo walionunua Zcash X Mighty Jaxx: Cypherpunk Zero Genesis Edition Toy 59.
72% ya ugavi (NFT 7,200) zitatolewa kwa umma kwa kutumia utaratibu mpya wa orodha ya walioidhinishwa unaohitaji matumizi ya pochi [wallet] ya Zcash inayotumia jumbe zilizosimbwa kwa usimbaji fiche [encryption] (maelezo zaidi hapa chini).
24% ya ugavi (NFT 2,400) utashikiliwa na ECC katika Akiba ya Cypherpunk, kwa matumizi katika mipango ya baadaye inayokuza Zcash na faragha [privacy] ndani ya eneo la Web3.
Ndiyo, mkusanyiko wa awali ulidukuliwa; mustakabali haujaandikwa.