MetaMask sasa inasaidia Zcash za faragha [shielded] (ZEC) kupitia Snap ya Zcash iliyotengenezwa na ChainSafe, ikikuwezesha kutuma, kupokea, na kusimamia ZEC za faragha moja kwa moja katika pochi yako [wallet] ya kivinjari. Ikiwa imekaguliwa na Hacken na kuorodheshwa katika Orodha rasmi ya Snaps ya MetaMask, haihitaji programu tofauti ya Zcash - ni MetaMask na Snap pekee.
Masharti ya Awali
Kiendelezi cha MetaMask (kompyuta ya mezani pekee) - Chrome, Edge, au Firefox.
Akaunti ya MetaMask - Maneno ya kurejesha pochi yamelindwa; Snap hupata funguo za Zcash kutoka kwayo.
Muunganisho Imara wa Intaneti - Kwa kusawazisha na mtandao wa Zcash.
Fedha - ETH ya kubadilisha [swap] kwa ZEC au kununua ZEC kutoka soko la kubadilishana sarafu [exchange].
Dokezo: Linda maneno yako ya kurejesha pochi ya MetaMask - yanadhibiti ETH na ZEC zote mbili.
https://zjs.zec.rocks ni seva ya lightwalletd inayooana na WebZjs (gRPC-web) inayoendeshwa na zec.rocks (@emersonian). Kwa testnet, tumia https://zjs.zec.rocks/testnet. Ukiendesha mwenyewe pochi ya wavuti ya WebZjs, hiki ndicho thamani ya kuweka kama LIGHTWALLETD_PROXY.
Tazama muhtasari wa akaunti yako ya Zcash, ikijumuisha:
Anwani zilizounganishwa na anwani ya uwazi [transparent]
Subiri usawazishaji ukamilike.
4. Weka Fedha kwenye Pochi Yako
Badilisha ETH -> ZEC - Tumia huduma kama LeoDex na utume kwenye anwani yako ya faragha. Utoaji kutoka Soko la Kubadilishana Sarafu - Toa ZEC uliyonunua kwenda kwenye anwani yako ya faragha ya WebZjs.
=> Tumia anwani za faragha (z) kwa faragha kamili [privacy].
5. Tuma / Pokea ZEC
Katika WebZjs, nenda kwenye Hamisha Salio.
Weka:
Code-highlight
- Shielded recipient address
- Amount
Thibitisha muamala [transaction] katika MetaMask (tia saini muamala).
Fedha zilizopokelewa zitaonekana katika WebZjs baada ya uthibitisho.
6. Thibitisha / Tatua Matatizo
Angalia WebZjs kwa masalio yaliyosasishwa (MetaMask haijaorodhesha ZEC moja kwa moja) .
Matatizo yakitokea:
Code-highlight
- Confirm you have the official ChainSafe Snap.
- Check correct network settings.
- Ensure correct address format.
- Reconnect via **Connect Snap** if needed.
Dokezo la Usalama: Sakinisha Snap ya ChainSafe iliyokaguliwa pekee; kagua ruhusa kabla ya kuidhinisha.
7. Angalia Vipengele vya Anwani
Nenda kwenye sehemu ya Pokea - Anwani yako Iliyounganishwa itaonyeshwa kwa chaguo-msingi.
Tumia toleo la hivi karibuni la MetaMask - toleo la umma linaunga mkono Snaps.
Mathibitisho ya faragha [shielded proofs] yanaweza kuchukua muda; WebAssembly hushughulikia ukokotoaji katika kivinjari.
Urejeshaji ni rahisi, sakinisha MetaMask na Snap, kisha leta maneno yako ya kurejesha pochi yaliyopo.
Snap hutumia ZEC za faragha kwa chaguo-msingi; anwani za uwazi si lengo kuu.
Tumia mainnet.zcashexplorer.app kwa uthibitisho wa miamala.