


Mfululizo: Zero to Zero Knowledge
Ikiwa unajifunza kuhusu Zcash kwa mara ya kwanza, utagundua kuwa kuna aina mbili za miamala zinazopatikana: Ya uwazi na Ya faragha.
Leo tunajifunza kuzihusu na kuchunguza mojawapo ya vipengele vipya katika mfumo ikolojia wa #Zcash, Anwani Zilizounganishwa.
Muamala wa Faragha hurejelea muamala wowote wenye anwani zilizosimbwa kwa mabwawa ya Sapling/Orchard.

Anwani Zilizounganishwa (UAs) zimeundwa kuunganisha miamala ya faragha au ya uwazi katika anwani moja.
Kuna aina 3 za anwani zinazotumika:
Idadi ya herufi (na hivyo ukubwa wa msimbo wa QR) huongezeka kwa kila aina.


Anwani na funguo husimbwa kama mfuatano wa baiti (Usimbaji Ghafi [Raw Encoding]).
Usimbaji wa Kipokezi [Receiver Encoding] hujumuisha taarifa zote muhimu za kuhamisha rasilimali kwa kutumia itifaki maalumu.
Usimbaji ghafi wa Anwani Iliyounganishwa ni mchanganyiko wa misimbaji (typecode, length, addr) ya vipokezi:
0x030x020x01Muhimu: Lazima kuwe na angalau anwani moja ya malipo ya faragha [shielded payment address] katika kila UA. (Anwani za Sprout hazitumiki tena baada ya boreshaji la Canopy.)

Uainishaji kamili: ZIP-316: Anwani Zilizounganishwa
Huu ni mabadiliko ya msingi ambayo tayari yanasaidia ZEC zaidi kuingia katika bwawa la faragha.
Orchard ilianzisha dhana mpya iitwayo Vitendo:
Daira anaeleza nafasi za Nanga (zcon3):
Katika baadhi ya hali (kwa mfano, miamala ya kuvuka mabwawa), kiasi kinaweza kuonekana kwa mwangalizi wa nje. Hata hivyo, valueBalanceSapling na valueBalanceOrchard hutumia commitment za homomorphic kuthibitisha jumla ya ZEC katika mabwawa ya faragha na kuzuia ughushi.
Soma zaidi: ZIP 209: Kataza Salio la Bwawa la Thamani ya Mnyororo Nje ya Masafa
Timu ya ECC inafanyia kazi mbinu mpya za RPC katika zcashd (ikichukua nafasi ya z_sendmany) ambazo zitawawezesha watumiaji kuhakiki mapema na kukubali/kukataa muamala uliopendekezwa kulingana na sifa zake za faragha.
Mfululizo huu hapo awali ulielekeza kwenye YWallet, kwa mpango wa muamala uliouonyesha kabla ya kubonyeza kutuma. YWallet haidumishwi tena na haitasasishwa kwa Ironwood, kwa hiyo haiwezi tena kufuata mnyororo [chain]. Badala yake, chagua pochi inayodumishwa kutoka kwenye ukurasa wa Pochi, na upendeleee ile inayokuambia muamala utafunua nini kabla haujatoka.
Makala bora kuhusu faragha ya miamala: https://medium.com/@hanh.huynh/
Mfululizo wa Asili wa ZecHub (@ZecHub)
https://x.com/ZecHub/status/1628498645627666432
Ukurasa huu ulikusanywa kutoka kwenye mfululizo wa asili wa Zero to Zero Knowledge kwa ajili ya wiki ya ZecHub.