



Karibu kwenye “PGP* (Sera Nzuri Sana) kwa Podikasti ya Crypto,” mpango wa Electric Coin Co.!
Tunachunguza makutano ya teknolojia ya blockchain, sera za umma [public policy], na mada za udhibiti za kimataifa. Lengo letu ni kuwapatia hadhira yetu maarifa ya kina na mitazamo ya wataalamu kuhusu masuala muhimu yanayounda mustakabali wa blockchain na sarafu-fiche [cryptocurrency].
Utasikia mahojiano na viongozi wa sekta, maafisa wa serikali, na wasomi walio mstari wa mbele katika kuunda mazingira ya sera za umma kwa teknolojia ya blockchain. Wageni wetu watashiriki mitazamo yao ya kipekee kuhusu changamoto na fursa zinazoikabili sekta hii, pamoja na athari za kanuni za sasa na zinazopendekezwa na mbinu za sera katika ukuaji na maendeleo ya mfumo ikolojia wa blockchain.