Pretty Good Privacy (PGP) ni kifurushi cha programu ya kriptografia kinachowezesha mawasiliano salama kupitia njia zisizo salama. PGP hutumia mchanganyiko wa usimbaji fiche [encryption] na sahihi za kidijitali ili kuhakikisha kwamba ni mpokeaji aliyekusudiwa pekee anayeweza kusoma ujumbe na kwamba mtumaji ndiye anayedai kuwa yeye.
Kuna vifaa [tools] vingi tofauti vya PGP vinavyopatikana, lakini baadhi ya vilivyo maarufu zaidi ni:
GnuPG (GPG): Kifaa cha mstari wa amri cha bure na cha chanzo huria cha OpenPGP. Chagua kifurushi au kiolesura cha picha kinachofaa kwa mfumo wako wa uendeshaji.
Thunderbird: Kiteja cha bure na cha chanzo huria cha barua pepe cha kompyuta ya mezani chenye usaidizi wa ndani wa OpenPGP tangu toleo la 78. Hahitajii Mailvelope ili kusimba barua pepe fiche.
Mailvelope: Kiendelezi cha kivinjari cha chanzo huria kinachoongeza OpenPGP kwenye huduma za barua pepe za wavuti zinazotumika, zikiwemo Gmail. Ni kifaa cha barua pepe za wavuti, si kiendelezi cha Thunderbird.
Baada ya kuzalisha jozi ya funguo za PGP, unaweza kuitumia kusimba fiche na kufumbua barua pepe. Ili kusimba fiche barua pepe, unahitaji kujua ufunguo wa umma wa mpokeaji. Kisha unaweza kutumia kifaa chako cha PGP kusimba fiche barua pepe kwa kutumia ufunguo wa umma wa mpokeaji.
Barua pepe iliyosimbwa fiche haitasomeka kwa mtu yeyote asiye na ufunguo binafsi wa mpokeaji. Ili kufumbua barua pepe, mpokeaji anaweza kutumia ufunguo wake binafsi kufumbua barua pepe.
Weka ufunguo wako binafsi salama. Ufunguo binafsi ni sehemu muhimu zaidi ya jozi yako ya funguo za PGP. Ikiwa mtu atapata ufunguo wako binafsi, anaweza kufumbua ujumbe wowote uliosimbwa fiche kwa kutumia ufunguo wako wa umma.
Shiriki ufunguo wako wa umma na watu unaowaamini. Unaweza kushiriki ufunguo wako wa umma kwa kuwatumia moja kwa moja, au kwa kuupakia kwenye seva ya funguo ya PGP.
Tumia nywila thabiti kwa pete yako ya funguo za PGP. Pete yako ya funguo za PGP ni faili inayohifadhi funguo zako za PGP. Ni muhimu kutumia nywila thabiti kulinda faili hii.
Sasisha programu yako ya PGP. Programu ya PGP husasishwa mara kwa mara ili kurekebisha hitilafu na kuboresha usalama. Ni muhimu kusasisha programu yako ili kuhakikisha unatumia vipengele vya hivi karibuni vya usalama.